Afisa wa ngazi za juu katika Baraza la Mpito la Libya amesema kuwa dikteta wa muda mrefu Kanali Muammar Gaddafi aliuawa na vijana wanamapinduzi waliomkamata. Akizungumza na kanali ya Aljazeera afisa huyo amesema kuwa Gaddafi alikuwa mjeuri kwa vijana hao na ujeuri wake ukawapandisha hasira vijana hao ambao waliamua kujichukulia sheria mikononi mwao. Inaaminika kuwa Gaddafi alipigwa risasi kichwani na miguuni. Wakati huo huo kwa siku ya pili mfululizo wananchi wa Libya wameendelea kumiminika katika ukumbi mdogo mjini Misrata ulikolazwa mwili wa marehemu Gaddafi ili kujionea wenyewe mabaki ya mtu aliyeitawala nchi yao kwa mkono wa chuma kwa miaka 42. Umoja wa Mataifa umelitaka Baraza la Mpito la Libya kuchunguza jinsi kiongozi huyo wa zamani alivyouawa
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 273677
Afisa wa ngazi za juu katika Baraza la Mpito la Libya amesema kuwa dikteta wa muda mrefu Kanali Muammar Gaddafi aliuawa na vijana wanamapinduzi waliomkamata